Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wakimbia Libya: UM

Maelfu wakimbia Libya: UM

Umoja wa Mataifa na washirika wake unaendelea kufuatilia taarifa za hivi karibuni za kuhama kwa wakimbizi wa ndani Magharibi mwa Libya, ikiwa ni kampeni ya miezi miwili dhidi ya dola ya kiislamu inayosababisha familia nyingi kukimbia eneo liitwal Sirte.

Tangu mwezi April na Mei, watu 35,000 wamekimbia Sirte, na kusababisha idadi ya wakimbizi wa ndani wenye asilia ya mji wa Pwani kufikia zaidi ya elfu 90, hiyo ikiwa ni zaidi ya robo tatu ya idadi ya jamii hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwezi ya hali ya kibinadmau nchini Libya, wengi wa wakimbizi wanasaka hifadhi katika miji kama vile Bani Walid, Tarhuna, Misratah na Al Jufrah huku idadi ndogo wakiyafikia maeneo mengine 15 ya Magharibi mwa nchi hiyo.

Ripoti hiyo inasema kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi wa ndani kunasababisha wenyeji kuhaha kutoa usaidizi ambapo kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ni mkimbizi mmoja kati ya asilimia 25 wanahisi utoshelevu wa mahitaji na asilimia 41 hawana huduma za ulinzi.