Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza kuu lajadili michezo na ujenzi wa amani

Baraza kuu lajadili michezo na ujenzi wa amani

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili ujenzi wa amani duniani kupitia michezo hususani michuano ya olimpiki. Joshua Mmali na taarifa kamili.

(TAARIFA YA MMALI)

Rais wa baraza kuu Mogen Lykketoft amewaambia wajumbe katika mkutano huo kuwa michuano ya olmpiki inayotarajiwa kuanza mnamo Agisti tano nchini  Brazil ni fursa nzuri kwa ulimwengu kutuma ujumbe wa amani na mshikamano.

Amezitaka nchi wanachama wa UM kutumia michuano ya Olimpiki kudhihirisha utamaduni wa amani na utulivu.

Kwa mara ya kwanza katika histioria timu ya wakimbizi  itashiriki katika michuano hiyo huku bendera ya Umoja wa Mataifa ikipepea katika michuano hiyo.

( SAUTI MOGENS)

‘‘Mashindano haya yataleta pamoja makundi kutoka kila pande ya dunia kwa ajili michezo, kama njia ya  kupigia chepuo amani, maelewano kati ya mataifa na watu.’’