Skip to main content

Ubanaji matumizi ya serikali kunadunisha hifadhi jamii- ILO

Ubanaji matumizi ya serikali kunadunisha hifadhi jamii- ILO

Shirika la Kazi Duniani (ILO), limesema kuwa ni asilimia 20 tu ya watu wote duniani ndio walio na hifadhi tosha ya jamii, kama vile malipo ya uzeeni au malipo wakati wanapoumwa, bima ya uzazi, na ya kukosa ajira.

Aidha, ILO imesema zaidi ya nusu ya idadi nzima ya watu duniani kamwe hawana bima ya aina yoyote ile.

Shirika hilo limesema serikali nyingi duniani zinabana matumizi zinapokabiliwa na shinikizo la bajeti, na hivyo kudunisha huduma zinazohakikisha hifadhi ya jamii.

Isabel Ortiz ni Mkurugenzi wa hifadhi ya jamii katika ILO

“Mnamo miaka ya 2008 na 2009, hifadhi ya jamii iliimarika, lakini mnamo mwaka 2010, nchi zilianza kubana matumizi, na hapo basi, hifadhi ya jamii ikaanza kuathiriwa, hususan katika nchi tajiri. Leo tunavyoongea, nchi 132 zinabana matumizi ya fedha kwa ajili ya umma, nyingi zaidi ni zenye maendeleo duni.”