Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji wa haki za binadamu Burundi kujadiliwa Geneva

Ukiukwaji wa haki za binadamu Burundi kujadiliwa Geneva

Kamati ya Umoja wa Mataifa inayopinga utesaji CAT, imeanza vikao vyake vya 58 leo mjini Geneva Uswisi, ambapo, hatua zilizochukuliwa na mataifa mbalimbali katika kuzuia na kuchukau hatua za kisheria dhidi ya watu waliohusika na vitendo vya utesaji vilivyofanyika katika nchi hizo zitajadiliwa.  Joseph Msami na taarifa kamili.

( TAARIFA YA MSAMI)

Kamati hiyo inatarajia kufanya tathimini maalum kuhusu Burundi, kufuatia taarifa ambazo imekuwa ikipokea za kuzorota kwa haki za binadamu nchini humo.

Mnamo Juali 28 hadi 29 wajumbe wa CAT pamoja na ujumbe wa Burundi ukiongozwa na waziri wa sheria, watajadili mambo kadhaa ambayo kamati iliomba ripoti hiyo mwaka jana Desemba kutoka kwa serikali ya  taifa hilo linalokabiliwa na machafuko.

Miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa ni pamoja na  hatua zilizochukuliwa kuchunguza mauaji, uwekwaji vizuizini, utesaji na matibabu kwa wanachama wa upinzani.

Kadhalika kamati hiyo ya kupinga utesaji CAT na wajumbe wa serikali ya Burundi watajadili hatua zilizofikiwa katika uchunguzi wa mashambulizi dhidi ya mwanaharakati wa haki za binadamu Pierre-Claver Mbonimpa mwezi Agosti mwaka jana pamoja na kutekwa na kuawa kwa mwanae Welly Nzitonda mwezi Novemba mwaka huo huo.