Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wahanga wa kiraia Afghanistan ilifikia rekodi mpya mapema 2016 -Ripoti

Idadi ya wahanga wa kiraia Afghanistan ilifikia rekodi mpya mapema 2016 -Ripoti

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeonyesha kuwa idadi ya raia waliouawa au kujeruhiwa nchini Afghanistan katika miezi sita ya kwanza ya 2016 iliweka rekodi mpya, tangu takwimu za wahanga wa kiraia nchini humo zilipoanza kuwekwa mnamo mwaka 2009.

Ripoti hiyo iliyochapishwa leo Julai 25, inaonyesha kuwa raia 5,166 waliuawa au kujeruhiwa katika miezi sita ya kwanza ya 2016, takriban theluthi moja kati yao wakiwa ni watoto.

Idadi nzima ya wahanga wa kiraia iliyorekodiwa tangu Januari 2009 hadi Juni 2016, imepanda hadi zaidi ya 60,000, vikiwemo vifo zaidi ya 22,000 na majeruhi zaidi ya 40,000.

Miongoni mwa wahanga wa mwaka huu ni watoto 1,509, ambapo 388 waliuawa na 1,121 kujeruhiwa.