Tisho la ugaidi bado linaendelea na ni kubwa: Laborde

22 Julai 2016

Tishio la ugaidi bado linaendelea , ni kubwa na ni la kuaminika amesema mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya kupambana na ugaidi (CTED). Jean-Paul Laborde ameyasema hayo akijiandaa kutoa taarifa kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa Ijumaa , kuhusu mada ya kuongezeka kwa wapiganaji magaidi wa kigeni kote duniani.

Mwezi September baraza la usalama lilipitisha azimio lililowataka nchi zote wanachama kuchukua hatua kali dhidi ya wapiganaji hao.

Kundi la kigaidi la ISIL au Daesh limefanya jumla ya mashambulizi 393 katika nchi 16 , mengi yakiwa nchini Iraq na Syria. Hivyo

(SAUTI YA LABORDE)

“Hivyo inamaanisha kwamba tishio hili halipungui na ni kutokana na kweli kwamba shinikizo kwa kundi kama Daesh kwa mfano ni kubwa kwa kiasi kwamba kundi hilo linarejea kwenye mashambulizi yake ya kigaidi, na uwezo wa kundi hilo ni mkubwa sana na wanaweza kufanya hivyo katika sehemu mbalimbali”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter