Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wawafikia watu 15, 000 walioathirika na machafuko Nigeria

Msaada wawafikia watu 15, 000 walioathirika na machafuko Nigeria

[caption id="attachment_253311" align="alignleft" width="300"]hapanapalenigeria

Msafara wa msaada nchini Nigeria umefikisha neema ya kuokoa maisha kwa watu 15,000 Kaskazini Mashariki mwa hiyo. Watu hao wamekimbia machafuko ya Boko Haram.

Kwa mujibu wa shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA msafara wa malori ya msaada uliwasili Alhamisi mjini Banki, jimbo la Borno baada ya kuvuka mpaka kutokea Cameroon.

Jimbo hilo bado si salama kwa kufikisha misaada hasa kutokea ndani ya Nigeria kama ananavyosema Jens Laerk msemaji wa OCHA

(SAUTI YA JENS LAERK)

“Hivi sasa operesheni za kuvuka mpaka ni za lazima, kwani hakuna fursa ya kuingia Maiduguri Nigeria; Maidugiri ni kama kitovu cha huduma za kibinadamu, kinachosaidia watu wengi waliotawanywa na mapigano na walioathirika katika jimbo la Borno ”

Msaada uliofikiwa ni tani 31 za chakula ambacho kitatosheleza watu hao kwa siku saba. Msaada huo umefika baada ya onyo la Umoja wa mataifa mapema wiki hii kwamba watoto 50,000 katika jimbo la Borno huenda wakafa na utapia mlo wasipopata msaada wa haraka.