Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa UNCTAD14 jijini Nairobi

Mkutano wa UNCTAD14 jijini Nairobi

UNCTAD, kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, imehitimisha mkutano wake wa 14 mjini Nairobi Kenya. Maudhui ya  mkutano huo yalikuwa kutoka maamuzi kwenda vitendo. Mikutano ya ngazi mbali mbali ilifanyika ikiwemo majukwaa ya vijana na mashirika ya kiraia. Viongozi wa nchi, halikadhalika na ile ya wawekezaji. Suala la bidhaa nalo liliangaziwa, ili hatimaye biashara ilenge kuleta maendeleo kwa kila mkazi wa sayari ya dunia. Je nini kilifanyika? Ungana basi na Joseph Msami kwenye makala hii.