IOM: Pendekezo la Trump kujenga ukuta kuzuia wahamiaji halisaidii

22 Julai 2016

Pendekezo la mgombea Urais Donald Trump la kujenga ukuta baina ya Marekani na Mexico limeelezwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, kuwa ni la kutia mashaka sana na halina matunda yoyote.

Matamshi hayo ya Ijumaa kutoka kwa mshirika wa Umoja wa mataifa yamekuja kufuatia hotuba ya Trump kwenye mkutano mkuu wa chama cha Republican Alhamisi usiku.

Katiba hotuba yake , mgombea huyo amezungumzia kujenga ukuta imara mpakani ili kuzuia wahamiaji haramu , magenge ya wahalifu na ghasia kuingia nchini Marekani. Joel Milliman ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JOEL MILMAN)

“Tuanhisi kwamba hulka na majaribio ya kujenga vizuizi na kuzuia uhamiaji hakuna faida, na kwamba inalazimisha watu kushirikiana na magenge yasiyojali ya uhalifu, ni hkunufaisha makundi hayo, inawapa rasilimali kviongozi wala rushwa katika pande zote za mpaka, popote mpaka huo ulipo "

Hii ni hali ambayo imekuwa kwenye muungano wa Ulaya kwa miaka mine iliyopita ameongeza Joel Milliman, ambako wanawazuia wahamiaji na wakimbizi kuingia katika baadhi ya nchi Kusini mwa Ulaya na kujikuta watu hao wanakwama mpakani.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter