Skip to main content

IFRC imezindua ombi kukabilia mlipuko wa homa ya manjano, surua na kipindupindu DRC

IFRC imezindua ombi kukabilia mlipuko wa homa ya manjano, surua na kipindupindu DRC

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu IFRC, kimezindua ombi la dharura la dola milioni 2.2 , ili kusaidia mapambano dhidi ya mlipuko wa magonjwa matatu nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC.

Maradhi hayo ni homa ya manjano inayoendelea, surua na kipindupindu. IFRC inasema homa ya manjano imeathiri mamia ya watu huku wengine wakipoteza maisha, wakati kipindupindu kimeshakatili maisha ya watu 94 na wengine 6000 wameathirika.

Kwa upande wa surua visa vilivyorokodiwa ni 744 na watoto 26 wamepoteza maisha. Shirikisho hilo linasema fedha zitasaidia katika kampeni ya kupita nyumba hadi nyumba kutoa matibabu, jancho, dawa na uelimishaji.