Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumeoanisha maono ya 2030 ya Kenya na SDGs- waziri Kiunjuri

Tumeoanisha maono ya 2030 ya Kenya na SDGs- waziri Kiunjuri

Wakati ripoti ya kwanza kabisa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu imezinduliwa jijini New York, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema ripoti hiyo ni taswira ya hali halisi ya hatua zilizopigwa duniani katika utekelezaji wa  ajenda ya mwaka 2030 malengo ya maendeleo endelevu.

Katibu Mkuu amesema takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kwamba mtu mmoja kati ya watu wanane anaishi katika umaskini uliokithiri, huku takriban milioni mia nane wakikabiliwa na njaa.

Aidha ameongeza kuwa watu bilioni 1.1 wanaishi bila umeme, na uhaba wa maji unaathiri zaidi ya watu bilioni 2.

Bwana Ban amesema hayo katika mkutano wa ngazi ya juu wa kisasa kuhusu maendeleo endelevu ambao umewakusanya mawaziri na wadau kutoka nchi mbali mbali.

Kenya ni miongoni mwa nchi ambazo zimewasilisha ripoti yake kwenye mkutano huo kupitia waziri wake wa ugatuzi, Mwangi Kiunjuri, ambaye amezungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii, akianza kwa kuelezea mikakati iliyowekwa nchini mwake.