Skip to main content

Utekelezaji wa SDGs unahitaji ushirikiano mkubwa: Ban

Utekelezaji wa SDGs unahitaji ushirikiano mkubwa: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuanza kwa safari ya miaka 15 inayoanza baada ya kuzinduliwa kwa ripoti ya kwanza ya maendeleo endelevu SDGs ni mwanzo mzuri lakini unaohitaji ushirikiano mkubwa.

Wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo mjini New York, Ban amesema familia ya Umoja wa Mataifa na wadau wake lazima wafanye kazi pamoja ili kufanikisha safari hiyo aliyoiita ya kihistoria.

Ban amewaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa wa jukwaa la siasa kuhusu maendeleo endelevu (HLPF) kuwa lazima kujifunza katika serikali, mamlaka za kitaifa, wafanyabiashara na asasi za kiraia na Umoja wa Mataifa ili kufikiri tofauti.

Mkutano wa HLPF umeanza mnamo Julai 11 na leo hii umekamilka kwa kuzinduliwa ripoti hiyo.