Hatua zichukuliwe dhidi ya ubakaji India:UNICEF

Hatua zichukuliwe dhidi ya ubakaji India:UNICEF

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limelaani vikali vitendo vya ubakaji dhidi ya wasicha nchini India na kutaka hatua zichukuliwe haraka kukomesha vitendo hivyo. Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa ya msichana mdogo kutoka Dalit India kubakwa na genge la watu watano, ambao pia walimbaka msicha huyohuyo miaka mitatu iliyopita.

Anju Malhorta mshauri mkuu wa masuala ya jinsia wa UNICEF amesema tukio hilo linadhihirisha utamaduni mbaya wa ukwepaji sheria katika masuala ya ukatili dhidi ya wasichana na wanawake. Amesema takribani wasichana milioni 120 kote duniani na msichana mmija kati ya 10 anakabiliwa na ukatili wa kingono katika maisha yake.

UNICEF inasema wengi wa wasichana hao wanakumbwa na ukatili huo kwa mara ya kwanza wakiwa na umri wa kati ya miaka 15 na 19, hivyo kusikitishwa tu haitoshi kinachotakiwa sasa ni hatua kukomesha hali hiyo iliyogeuka mazoea na kuwatendea haki na kuwapa ulinzi unaostahili wahanga wa vitendo hivyo.