Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msukumo mpya wa kimataifa umezinduliwa kuziba pengo la tiba ya HIV kwa watoto

Msukumo mpya wa kimataifa umezinduliwa kuziba pengo la tiba ya HIV kwa watoto

Wadau mbalimbali wanaojihusisha na matibabu ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa watoto, wameungana kwenye mkutano wa 21 wa ukimwi unaofanyika Durban Afrika Kusini, kuzindua msukumo wa haraka wa kimataifa ili kutokomeza ukimwi kwa watoto ifikapo mwaka 2020. Flora Nducha na taarifa zaidi

(TAARIFA YA FLORA)

Mkutano huo maalumu umejikita katika kufikia lengo la kimataifa la kuhakikisha watoto takribani milioni 1.6 wanapata fursa ya dawa za kupunguza makali ya ukimwi ifikapo mwaka 2018.

Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO na lile la kukabiliana na masuala ya ukimwi UNAIDS, ongezeko la kuzuia maambukizi ya HIV miongoni mwa watoto limeweka msingi wa kutokomeza ukimwi, muongo mmoja mapema zaidi ya lengo la kimataifa.

Hata hivyo WHO imeonya kwamba ili kutokomeza ukimwi kwa watoto, juhudi za kuzuia lazima ziende sanjari na mahitaji ya tiba kwa watoto wanaoishi na VVU.