Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imeanza operesheni za dharura za ugawaji chakula Malawi

WFP imeanza operesheni za dharura za ugawaji chakula Malawi

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, limeanza operesheni mpya za kuokoa maisha nchini Malawi. Kwa mujibu wa shirika hilo watu wapatao milioni 6.5 karibu asilimi 40 ya watu wote huenda wakahitaji msaada wa chakula katika miezi ijayo.

Operesheni hiyo itakuwa moja ya operesheni kubwa kabisa za msaada wa chakula wa dharura kuwahi kufanyika katika historia ya taifa hilo. Malawi ni moja ya nchi za Kusini mwa Afrika zilizoathirika vibaya na ukame uliosababishwa na athari za El Niño.