Skip to main content

Kenya yatakiwa kuhakikisha uhuru wa mamlaka ya nishati ya atomiki- IAEA

Kenya yatakiwa kuhakikisha uhuru wa mamlaka ya nishati ya atomiki- IAEA

Timu ya wataalam wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), imeitaka Kenya ihakikishe uhuru wa mamlaka ya nishati hiyo nchini humo, ili kuiwezesha mamlaka hiyo kutimiza jukumu lake la kuimarisha uamuzi unaohusiana na vituo vyote vyenye mnururisho wa mionzi ya nyuklia.

Timu hiyo imetoa wito huo mwishoni mwa ziara yake ya siku kumi nchini Kenya, ambayo ililenga kufanyia tathmini mkakati wa usalama wa minururisho nchini humo.

Kiongozi wa timu hiyo, Javier Zarzuela, amesema Kenya imeonyesha dhamira ya kuimarisha mkakati wake wa kitaifa wa usalama wa nyuklia kisheria, lakini akaongeza kuwa kuchukua hatua za kuhakikisha uhuru wa bodi inayosimamia minururisho kutaisaidia kutimiza lengo la kuhakikisha usalama zaidi.

Kenya hutumia minururisho ya nyuklia katika vituo vya afya, utafiti na viwandani, na inatazamia kutumia nishati ya nyuklia katika kutimiza mahitaji yake ya nguvu za umeme.