Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yachagiza nchi kuchukua hatua kupunguza vifo vya homa ya ini

WHO yachagiza nchi kuchukua hatua kupunguza vifo vya homa ya ini

Nchi zimechagizwa kuchukua hatua haraka kuboresha ufahamu kuhusu homa ya ini, kuongeza fursa ya kufanyiwa vipimo na kupata huduma ya tiba.

Wito huo umetolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO, katika ujumbe wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya homa ya ini, ambayo huadhimishwa Julai 28 kila mwaka.

Shirika hilo linasema hivi leo mtu mmoja kati ya 20 walio na virusi vya homa ya ini ndiye anatambua kuwa anavyo, na mtu mmoja kati ya 100 walio na homa hiyo ndiye anayetibiwa.

Duniani kote watu milioni 40 wameambukizwa homa ya ini aina B na C, ikiwa ni mara 10 zaidi ya watu wanaoishi na VVU.

Dkt. Stefan Wiktor, ni mkuu wa programu ya kimataifa kuhusu homa ya ini katika WHO.

(Sauti ya Dkt. Stefan Wiktor)

 “Hakika homa ya ini ni tatizo kubwa la afya kimataifa , tunakadiria kwamba watu wapatao milioni 400 wanaishi na homa ya ini aina B na C na vifo milioni 1-45 vya homa hiyo vimetokea mwaka 2013.”