Ushirikishaji wa umma ni moja ya mikakati ya Kenya katika kufikia SDGs- Waziri Kiunjuri
Mikakati imewekwa ili kuhakikisha kwamba malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) yanafikiwa ifikapo mwaka 2030 nchini Kenya.
Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Kenya kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa kisiasa kuhusu maendeleo endelevu, unaondelea hapa jijini New York, ukilenga kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma.
Akizungumza na Idhaa hii mara tu baada ya kuwasilisha ripoti kwa niaba ya nchi yake, Waziri wa Ugatuzi wa Kenya, Mwangi Kiunjuri, amesema nchi yake iko katika mstari sahihi kwani kando na mipango inayonuia kuimarisha maswala ya usawa wa kijinsia na kukabiliana na umaskini na njaa ….
(sauti ya Kiunjuri )
Halikadhalika akataja umuhimu wake…
(Sauti ya Kiunjuri )