Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatutasaini mikataba tukiwa tumefumba macho- Tanzania

Hatutasaini mikataba tukiwa tumefumba macho- Tanzania

Mkutano wa 14 wa kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD ukiwa umeingia siku ya Nne, mjini Nairobi, Kenya, nchi wanachama wa kamati hiyo zimekuwa zikijadili makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi, EPA huku Tanzania ikisisitiza kuwa haitasaini mikataba ikiwa imefumba macho. Ripoti kamili na Assumpta Massoi kutoka Nairobi.

(Taarifa ya Assumpta)

Suala la mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi, EPA limekuwa likipatiwa kipaumbele katika mkutano wa 14 wa UNCTAD, ikielezwa kuwa ni moja ya njia za kuwezesha nchi zinazoendelea kujikwamua kutoka umaskini.

Hata hivyo kutoka nchi zinazoendelea kumekuwepo na wasiwasi pengine ni mtego na katika kusaini mikataba hiyo kumekuwepo na kusuasua. Charles Mwijage, Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Tanzania.

(Sauti ya Mwijage)

Na anazungumziaje msimamo wa Tanzania kuhussu mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Muungano wa Ulaya, EU?

(Sauti ya Mwijage)

Mkataba wa EPA kati ya EU na EAC ulikuwa utiwe saini Julai 18 mwaka huu.