Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yakabiliana na shuku ya mlipuko wa kipindupindu Sudan kusini

IOM yakabiliana na shuku ya mlipuko wa kipindupindu Sudan kusini

Timu ya madaktari wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, linakabiliana na mlipuko wa visa vinavyoshukiwa kuwa kipindupindu Juba Sudan Kusini.

Timu hiyo inatoa huduma ya dharura ya afya kwa watu waliotawanywa na machafuko ya wiki iliyopita katika mji huo mkuu.

Mapema wiki hii wizara ya afya ya Sudan Kusini ilitoa tahadhari baada ya mtu mmoja kufariki dunia na visa vingine 30 vinavyoshukiwa kuwa kipindupindu mjini Juba.

Visa 13 kati ya hivyo 30 vimebainika kuwa ni vya kipindupindu baada ya vipimo vya awali , ingawa vipimo zaidi vinafanyika kuthibitisha hilo. Visa vingine vimeripotiwa kata za Duk Terekeka.