Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za binadamu zizingatiwe wakati wa kudhibiti upinduaji wa serikali ya Uturuki: Zeid

Haki za binadamu zizingatiwe wakati wa kudhibiti upinduaji wa serikali ya Uturuki: Zeid

Kamishna mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amezitaka mamlaka nchini Uturuki kulinda haki za binadamu wakati wa kushugulikia jaribio la kupinduliwa kwa serikali nchini humo.

Katika taarifa yake mjini Geneva Uswisi, Zeid amenukuliwa akisema mamlaka za Uturuki zinapaswa kuimarisha tasisi za kidemokrasia na uwiano.

‘‘Nasikitishwa na vifo vya watu mwishoni mwa juma na kutuma salamu zangu za rambirambi kwa familia za wale waliouawa ". Amesema Zeid.

Ameitaka Uturuki kutekeleza utawala wa sheria kwa kusema kuwa wanaoawajibika na machafuko wafikishwe katika vyombo vya sheria kwa heshima na misingi ya sheria za kimahakama.

Watu wa Uturuki walimiminika mitaani mwishoni mwa juma wakitetea nchi yao kinyume na kundi walilolitumuhumu kuwa linakandamiza demokrasia yao.