Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya kususia mkutano wa AU, Burundi iko tayari kwa mazungumzo ya amani

Licha ya kususia mkutano wa AU, Burundi iko tayari kwa mazungumzo ya amani

Serikali ya Burundi imeutaka muungano wa Afrika kupata suluhu ya mvutano baiana ya Burundi na Rwanda, huku waziri wa mambo ya nje wa Burundi Alain Aime Nyamitwe akisema Serikali ya Burundi iko tayari kuendeleza mazungumzo ya amani.Kutoka Bujumbura, Muandishi wetu Ramadhani KIBUGA ana taarifa zaidi.

(TAARIFA YA KIBUGA)

Akielezea sababu ya Burundi ya kususia Mkutano wa kilele wa Muungano wa Afrika mjini Kigali mapema wiki hii, waziri wa Burundi wa mambo ya nje Alain Aimee Nyamitwe amesema serikali ilikusudia kutoa ujumbe kwa shirika hilo kuwa kuna haja ya kuushughulikia haraka mzozo kati ya Bdi na Rwanda kwa manufaa ya nchi mbili.

Kuhusiana na mazungumzo ya amani yaliyofanyika hivi karibuni mjini Arusha Tanzania , waziri wa mambo ya nje Alain Aime Nyamitwe amesema serikali iko tayari kwa mazungumzo lakini amekariri tena msimamo wa serikali kuwa hawatojadiliana na watu waliojaribu mapinduzi na kusimamia vurugu.

Muwakkilishi wa katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Burundi Jamal Ben Omar amezitaka pande zote kuweka mbali maslahi ya nchi na kufikia amani kumaliza mzozo wa kisisasa uliodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kugharimu vifo vya watu zaidi ya 500 huku raia laki moja na elfu sabini wakichukua hifadhi katika nchi jirani.

Mimi ni Ramadhani KIBUGA, Redio ya Umoja wa Mataifa, Bujumbura.