Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yataka nchi ziongeze kasi ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza

WHO yataka nchi ziongeze kasi ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imemulika haja ya kuongeza juhudi za kitaifa ili kutimiza malengo ya kimataifa ya kuwalinda watu kutokana na magonjwa ya moyo, saratani, kisukari na magonjwa ya mapafu.

Ripoti hiyo ya WHO imesema magonjwa hayo manne yasiyo ya kuambukiza, ndiyo yanayosababisha vifo vingi zaidi miongoni mwa watu wenye umri chini ya miaka 70, na hivyo kuwa tishio kubwa kwa maendeleo endelevu.

Licha ya hayo, utafiti huo uliotathmini uwezo wa kila taifa katika kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza, umebainisha kuwa baadhi ya nchi zinapiga hatua kubwa. Huku zingine zikichukua hatua za kulinda watu kutokana na matumizi ya tumbaku, vileo vya pombe, mlo unaodunisha afya, na kutofanya mazoezi.