Hatua zimepigwa lakini bado watu milioni 20 hawapati huduma ya HIV wanayostahili:Ban

18 Julai 2016

Ingawa hatua kubwa zimepigwa katika vita dhidi ya HIV na ukimwi, bado kuna watu milioni 20 ambao hawana fursa ya dawa za kupunguza makali ya ukimwi na wengine milioni 13 hawapati huduma inayostahili. Grace Kaneiya na taarifa kamili

(TAARIFA YA GRACE)

Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye mkutano wa 21 wa kimataifa wa ukimwi unaofanyika mjini Durban Afrika Kusini. Ban amesema ingawa watu wanaopata dawa za kupunguza makali ya ukimwi wameongezeka mara 17 na nchi zingine hawana watoto wanaozaliwa na virusi vya HIV, bado watoto wengi wanaoishi na virusi hivyo hawapati matibabu.

Hivyo ametoa wito

(SAUTI YA BAN)

“Kutokomeza maradhi haya, ni lazima tuzibe pengo ambalo linawafanya watu wasipate fursa ya huduma na kuishi kwa heshima, ni lazima tunapanue wigo wa rasilimali, sayansi na huduma. Tukifanya hivi tutamaliza unyanyapaa na ubaguzi, tutazuia kuenea kwa HIV na kuokoa maisha”

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter