Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu waanza kurejea makwao Sudan Kusini:OCHA

Watu waanza kurejea makwao Sudan Kusini:OCHA

[caption id="attachment_289379" align="alignleft" width="350"]hapanapaleunmiss

Ikiwa leo ni siku ya nne ya usitishaji uhasama mjini Juba Sudan Kusini , watu wengi wameanza kurejea majumbani kwao.

Kwa mujibu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA wahudumu wa misaada ya kibinadami hivi sasa wameyafikia maeneo yote ya watu waliotawanywa na machafuko ya hivi karibuni na kukadiria kwamba watu karibu 8000 bado wametaanywa na machafuko wakiwemo 4300 wanaohifadhiwa kwenye maeneo ya mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini UNMISS, na wengine 3700 nje ya maeneo hayo.

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanaendelea kutoa msaada wa dharura kwa wanaouhuitaji hasa wa maji safi ya kunywa, biskuti za kuongeza nguvu, lishe kwa watoto, vifaa vya kujisafi kama sabuni, kusaidia familia kuungana na waliopotezana, kugawa tena madawa, huduma za afya na vifaa vingine visivyo chakula.