Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti wabaini watoto zaidi ya milioni 260 hawako shule: UNESCO

Utafiti wabaini watoto zaidi ya milioni 260 hawako shule: UNESCO

Utafiti uliofanywa kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa kushirikiana na taasisi ya kimataifa ya takwimu na tathmini ya elimu EGM unaonyesha kuwa watoto zaidi ya milioni 260 hawako shuleni.

Kwa mujibu wa utafiti huo takwimu hii ni sawa na robo ya idadi ya watu barani Ulaya ambapo, watoto zaidi ya milioni 60 ni wale walioko kati ya umri wa miaka sita hadi 11, huku wengine zaidi ya milioni 140 wakiwa ni umri wa kuwa shule ya sekondari yaani kati ya miaka 15-17.

UNESCO hatua hii inatishia uwezekano wa kutumiza lengo namba nne la maendeleo endelevu SDGs la elimu bora hususani katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Akizungumzia utaifiti huo Katibu Mkuu wa tume ya taifa ya UNESCO nchini Tanzania Dk Moshi Kimizi ameshauri kile kinachopaswa kufanywa.

(SAUTI KIKMIZI)