Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya Nigeria, SheTrades yazinduliwa Kenya

Baada ya Nigeria, SheTrades yazinduliwa Kenya

Kituo cha biashara cha kimataifa, ITC kwa kushirikiana na serikali ya Kenya na benki ya Barclays, leo wamezindua mpango wa kuwezesha wajasiriamali wanawake nchini humo kupenyeza masoko ya kimataifa ili hatimaye kujikwamua kutoka lindi la umaskini. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Mpango huo uitwao SheTrades Kenya, unalenga kuunganisha wanawake Elfu Kumi nchini humo huku kimataifa ikilenga wanawake Milioni Moja ifikapo mwaka 2020.

Arancha Gonzales ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITC ambayo ni taasisi tanzu ya UNCTAD na WTO.

(Sauti ya Arancha)

"Kwa kuanzia na uwezo wao wa kujiunga na mtandao wa SheTrades.com, jukwaa la kimataifa linalounganisha wanawake wajasiriamali duniani ili hatimaye wawe na ushirika thabiti na ndipo kwa pamoja wakiwa wanunuzi na wauzaji waweze kuunda uchumi thabiti."

Wakati wa uzinduzi, wanawake wajasiriamali wanufaika wa SheTrades Kenya walionyesha bidhaa zao na miongoni mwao ni kampuni ya ubunifu wa mitindo Akinyi Odongo Kenya ikiwakilishwa na Matilda King'oria..

(Sauti ya Matilda)