Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio la kigaidi, Nice, Ufaransa

Ban alaani shambulio la kigaidi, Nice, Ufaransa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani shambulio la kigaidi la Julai 14 mjini Nice, Ufaransa ambalo lilitekelezwa wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku Kuu ya kitaifa ya Bastille.

Ban amepeleka salamu za rambi rambi kwa familia za wahanga, serikali na watu wa Ufaransa, huku akiwatakia uponaji haraka waliojeruhiwa.

Taarifa ya msemaji wake imeeleza matarajio ya Katibu Mkuu kuwa waliohusika katika mauaji hayo watatambuliwa haraka na kufikishwa mbele ya sheria.

Aidha, ameelezea mshikamano wake na serikali ya Ufaransa na watu wake wakati wanapokabiliana na tishio hilo la kigaidi, na kusisitiza haja ya kuongeza juhudi za kikanda na kimataifa katika kupambana na ugaidi na itikadi kali katili.