Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

#UNCTAD14 vijana wajumuishwa, wanawake kuangaziwa- Dkt. Kituyi

#UNCTAD14 vijana wajumuishwa, wanawake kuangaziwa- Dkt. Kituyi

Baada ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kupitisha makubaliano kadhaa muhimu mwaka jana ikiwemo ajenda ya maendeleo endelevu na mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, kauli muhimu hivi sasa ni kwamba hakuna anayepaswa kuachwa nyuma. Kila mkazi wa sayari ya dunia awe mwanamke, mwanaume, mtoto au mzee anapaswa kujumuika na kujumuishwa kwenye mipango ya maendeleo kwa ustawi wa wote.

Harakati zinaendelea na kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na maendeleo, UNCTAD nayo haiko nyuma. Imeanza kuchukua hatua na juhudi zaidi zitaimarika kwenye mkutano wake wa 14 utakaoanza Jumapili hii huko Nairobi, Kenya. Matarajio ni yapi? hatua gani zinalenga kumkomboa mwanamke? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Katibu Mkuu wa UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi mjini Nairobi, ambaye katika sehemu hii ya kwanza ya mahojiano ameshukuru Kenya kwa kuwa mwenyeji na pia ametaja kile kinachotarajiwa.