Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP yakagua athari za utupaji taka zenye sumu Abidjan, Côte d'Ivoire

UNEP yakagua athari za utupaji taka zenye sumu Abidjan, Côte d'Ivoire

Kufuatia ombi la serikali ya Côte d'Ivoire, Shirika la Mpango wa Mazingira, UNEP, linafanya tathmnini huru katika maeneo ya mji mkuu Abidjan yaliyoathiriwa na utupaji taka zenye sumu kutoka meli ya Probo Koala mnamo mwaka 2006. Taarifa kamili na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Kazi ya UNEP ya ukaguzi wa maeneo hayo ilifanywa na timu ya wataalam mseto wa kimataifa na kitaifa kati ya Julai 4 na Julai 14 mwaka huu wa 2016.

Timu hiyo ilichukua sampuli za udongo, maji, hewa, mimea, samaki na mabaki mengine kutoka maeneo zilikotupwa taka hizo na maeneo jirani, na kuzipeleka katika vituo vitatu tofauti vya mahabara ya kimataifa barani Ulaya kufanyikwa tathmini.

Matokeo ya tathmini hizo yatalinganishwa na yale ya viwango vya kitaifa nchini Côte d'Ivoire, pamoja na viwango vya mwongozo wa kimataifa, na kisha UNEP itachapisha ripoti ya kina kufikia Disemba mwaka huu.