Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna aliyewajibishwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu Ukraine:UM

Hakuna aliyewajibishwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu Ukraine:UM

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa Alhamisi inatanabaisha mauaji yaliyojiri Ukraine tangu Januari 2014 na ambavyo hakuna aliyewajibishwa na uhalifu huo. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na kitengo cha ufuatiliaji haki za binadamu cha Umoja wa Mataifa nchini Ukraine inasema vita vya silaha katika baadhi ya wilaya za Donetsk na Luhansk, vilichochewa na wapiganaji wa kigeni na silaha zilizoingizwa kutoka Urusi, na hivyo kusababisha ukiukaji mkubwa wa haki za watu za kuishi nchini Ukraine kwa miaka miwili iliyopita ambapo zaidi ya watu 2000 wamepoteza maisha na wengine kwa maelfu kujeruhiwa .

Kikubwa zaidi ripoti inasema ukwepaji wa sheria kwa mauaji hayo umetawala hali inayowashajihisha watendaji uhalifu kuendelea na kuzima matumaini ya kupatikana kwa haki. Cecile Pouilly ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva

(SAUTI YA CECILE )

"Mashambulizi ya kimataifa dhidi ya raia yanaweza kuchukuliwa kama uhalifu wa kivita  na mauaji  ya raia ambao hawakushiriki vita kama wauaji. Pia ripoti imeainisha kwamba, watu wachache sana wanaowajibishwa na mauaji haya na hakuna aliyebeba jukumu hilo la mauaji ya raia, ambayo ni matokeo ya vita vilivyofanyika Mashariki mwa nchi hiyo."