Ahadi yetu kukwamua wajasiriamali wanawake inazaa matunda- Dkt. Kituyi
Hatua zilizochukuliwa na kamati ya kimataifa ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD kupatia kipaumbele wanawake kwenye biashara na maendeleo zimeanza kuzaa matunda na kudhihirisha kuachana na maneno kwenda kwenye vitendo.
Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa, mjini Nairobi, Kenya kunakotarajiwa kuanza mkutano wa 14 wa kamati hiyo, Katibu Mkuu wa UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi ametolea mfano uwezeshaji wanawake wajasiriamali wa mboga za majani nchini Tanzania kuweza kuuza bidhaa hizo kwenye hoteli za kitalii.
(Sauti Dkt. Kituyi)
Ametaja hatua nyingine ni kuhakikisha wanawake wanashiriki kwenye mikutano na kuwasilisha mada ambapo kwenye mkutano huu...
(Sauti ya Dkt. Kituyi)