Ushirika mzuri baina ya sayansi na sera unahitajika kufikia SDG’s-Ripoti

Ushirika mzuri baina ya sayansi na sera unahitajika kufikia SDG’s-Ripoti

[caption id="attachment_282904" align="alignleft" width="449"]hapanapalesgds

Uelewa wa misingi ya kisayansi katika kuchukua hatua utahitajika ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDG’s ifikapo mwaka 2030 imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na Umoja wa mataifa wakati wa kongamano la ngazi ya juu kuhusu maendeleo endelevu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya 2016 ya SDG’s vipengee muhimu kwa ajenda ya mwaka 2030 kama kitahitajika nini kuhakikisha kwamba hakuna atakayesalia nyuma , bado hilo halijatafitiwa kisayansi.

Ripoti imebaini kwamba ajenda mpya inahitaji kuuliza maswali tofauti tofauti na mengi hayana majibu ya kitafiti.

Ripoti hiyo iliyojikita kwenye tathimini ya kisayansi zaidi katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu, imeandaliwa na idara ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na maendeleo ya kijamii na imejumuisha utaalamu wa kiufundi wa wanasayansi na wataalamu 245.

Ripoti imesisitiza ni muhimu kutambua ni nani aliyeachwa nyuma, hasa watu masikini, wasiojumuishwa,wanaobaguliwa na wasiotendewa usawa ili sera za kuzuia hayo ziweze kuwekwa.