Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wagombea nafasi ya Katibu Mkuu wa UM kushiriki mjadala mbashara

Wagombea nafasi ya Katibu Mkuu wa UM kushiriki mjadala mbashara

Wagombea wa nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wanatarajiwa kukabiliwa na changamoto katika mjadala mbashara kupitia televisheni katika ukumbi wa mikutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York Jumanne katika mjadala.

Wagombea 12 wameteuliwa kugombea nafasi hiyo ili kumrithi Katibu Mkuu wa sasa Ban Ki-moon atakayemaliza kipindi chake cha uongozi mwishoni mwa mwaka huu.

Awali mchakato wa kumpata Katibu Mkuu uliukwa unafanyika kwa siri lakini kwa sasa uwazi na demokrasia vimetawala mchakato huo.

Dan Thomas ni msemaji wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

(SAUTI DAN)

‘‘Hii ni fursa kwao ya mwisho ya kuwahamasisha nchi wananchama na dunia kwa ujumla. Nafikiri wanasubiri kwa hamu, ni mazingira ya changamoto kwani ni mjadala mbashara kupitia televisheni . Kwahiyo inawabidi waongee kwa sauti ya hamasa na wazungumze mada zao haraka.’’