Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inaimarisha msaada wake Sudan Kusini

WHO inaimarisha msaada wake Sudan Kusini

Shirika la afya duniani WHO limesema linaimarisha uwezo wake, fedha wafanyakazi na rasilimali zingine ili kukabiliana na mahitaji ya haraka ya kibinadamu kufuatia zahma inayoendelea Sudan kusini.John Kibego na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA KIBEGO)

Shirika hilo linasema kina mama wakiwa wamebeba watoto wao wameonekana wakikimbia vita kusaka ulinzi kwenye kituo cha Umoja wa mataifa ambako hivi sasa eneo hilo limezuiliwa na vikundi hasimu na matokeo yake maelfu ya watu wamearifiwa kukwama kwenye makanisa na shule wakiwa na familia zao bila huduma za afya, maji na vifaa vya kujisafi.

Sudan Kusini ni moja ya nchi zenye idadi kubwa ya vifo vya wajawazito duniani, kwa mujibu wa WHO, Benki ya dunia na Shirika la idadi ya watu duniani UNFPA idadi ya vifo vya wajawazito ni 730 kwa kila 100,000, na watoto wachanga 1900 hufa kila mwaka

Tarik Jasarevic ni msemaji wa WHO

(SAUTI YA TARIK)

"WHO imeimarisha juhudi kwa kuwekeza raslimali zaidi ikiwemo nguvu kazi ili kukabiliana vilivyo na janga la kibindamua linaloshuhudiwa kufuatia mzozo unaoendelea."