Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fuko la UM la ujenzi wa amani kufadhili miradi ya miundombinu Somalia:

Fuko la UM la ujenzi wa amani kufadhili miradi ya miundombinu Somalia:

Kwa mara ya kwanza kwa Umoja wa mataifa, fuko la Umoja wa mataifa la ujenzi wa amani , limesema litapeleka fedha kwa mfuko wa ufadhili wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Somalia. Fedha hizo zitaingizwa kwenye bank kuu ya Somalia ili kufadhili miradi ya miundombinu , kati juhudi za kuimarisha mifumo ya taifa hilo, umetangaza leo mfuko wa ufadhiili wa ujenzi wa amani PBF.

Kwa mujibu wa mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Somalia Peter de Clercq, hatua hiyo ni kubwa na ya kihistoria katika juhudi za kuimarisha mifumo ya kitaifa na kuiwezesha serikali ya shirikisho ya Somalia kuinua uwezo wake na uhalali wake kwa raia wa nchi hiyo.

Miradi hiyo ya majaribuo itagharimu dola milioni 2 katika maeneo ya Lower Jubba, Benadir na jimbo jingine ambalo bado halijachaguliwa. Fedha hizo kutoka PBF zinaingizwa kwenye bank kuu ya Somalia kupitia mfuko wa dhamana wa washirika mbalimbali wa Umoja wa mataifa ambao pia utakuwa ukitoa taarifa kuhusu bajeti ya serikali amesema de Clercq.