Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyakula vya ziada Rio kunufaisha wahitaji

Vyakula vya ziada Rio kunufaisha wahitaji

Kuelekea mashindano ya olimpiki ya majira ya kiangazi huko Rio de Janerio nchini Brazil, mradi maalum umeanzishwa ili kuhakisha vyakula vya ziada havitupwi, bali vinakusanywa na kupatiwa wahitaji.

Mpango huo umetangazwa leo huko Roma, Italia mbele ya mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva, ukipatiwa jina la Reffeto-Rio.

Kupitia mpango huo, vyakula vya ziada kutoka kijiji cha olimpiki, vitakusanywa na hatimaye wapishi bora duniani watavibadilisha kuwa mlo na lishe bora.

Wapishi watatumia fursa hiyo kupatia mafunzo vijana juu ya mapishi bora ambapo watu wamealikwa kujitolea sambamba na wapishi mashuhuri 45 kutoka maeneo mbali mbali duniani.

Mradi wa Reffeto-Rio unatokana na mradi wa aina hiyo uliobuniwa wakati wa maonyesho ya Milano mwaka jana.