Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya hatua za usalama Boko Haramu bado ni tishio Nigeria:Lanzer

Licha ya hatua za usalama Boko Haramu bado ni tishio Nigeria:Lanzer

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa na mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Nigeria Toby Lanzer, amesema licha ya hatua kubwa za kiusalama kundi la Boko Haram bado linaendelea kuhatarisha usalama na kutishia maisha ya mamilioni ya watu.

Lanzer anasema asilimia 90 ya wato haoa ambao sasa wanaishi katika sintofahamu walikuwa wakiishi kwa kutegemea kilimo, uvuvi na ufugaji.Lanzer ameyasema hayo baada ya kufanya ziara sita katika sehemu mbalimbal;I za jimbo la Bono nchini Nigeria.

Amesema katika ziara hiyo ameshuhudia madhila yanayowakabili maelfu ya watu ambao wengi wanaendelea kufungasha virago na kukimbia. Hadi kufikia Leo hii watu milioni 4.4 hawana uhakika wa chakula Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, na kwa kuwasikiliza wavulana , wasichana , wanachama wa makundi ya vijana na wazee katika miji ya Dikwa and Monguno Lanzer amesema kumetanabaisha madhila yasiyoelezeka ambayo yanawakabili watu hawa kwa miaka mitatu sasa.

Baadhi ya madhila hayo ni kutokuwepo usalala, vijiji kuchomwa moto, wavulana na wanaume kuuawa, na kina dada na mabinti kubakwa.