Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya raia watu 6,000 wa CAR wakimbilia Chad na Cameroon

Zaidi ya raia watu 6,000 wa CAR wakimbilia Chad na Cameroon

Ghasia mpya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR zimesababisha watu zaidi ya Elfu Sita kukimbilia nchi jirani za Chad na Cameroon.

Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR limesema ghasia hizo baina ya wakulima na wafugaji kaskazini magharibi mwa nchi zilianza katikati mwa mwezi uliopita na kuna hofu kuwa hali itakuwa mbaya zaidi.

Wafanyakazi wa UNHCR kusini mwa Chad wamesaidia serikali kusajili zaidi ya wakimbizi Elfu Tano kwenye vijiji vya Sourouh na Mini mpakani na CAR.

Idadi kubwa ya wanaokimbia ni wanawake, watoto na wazee, ingawa yaripotiwa kuwa wanaume nao wanakimbizi na kuacha shughuli zao za kuwapatia kipato.