Skip to main content

Umoja wa Mataifa walaani mauaji dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika

Umoja wa Mataifa walaani mauaji dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika

Kikundi kazi cha wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za Wamarekani wenye asili ya Afrika kimelaani mauaji dhidi ya raia wawili wa jamii hiyo yaliyotekelezwa na askari. Flora Nducha na maelezo kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Katika tamko lao wataalamu hao wamesema mauaji dhidi ya Philando Castile wa jimboni Minnesota na Alton Sterling wa Louisiana ambayo yamesambazwa kupitia video hayawezi kupuuzwa na kutaka uchunguzi huru ili kuhakikisha watekelezaji wanafikishwa mahakamani na kuadhibiwa.

Kikundi kazi hicho kadhalika kimelaani mauaji dhidi ya askari huko Dallas na kutaka watekelezaji wawajibishwe.

Wamesema utumiaji wa nguvu kupitiliza dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika ni matukio endelevu kwani mara nyingi huripotiwa kuuawa mara mbili zaidi ya kiwango cha mauaji dhidi ya weupe.