Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kujadili suluhu ya wakimbizi na wahamiaji

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kujadili suluhu ya wakimbizi na wahamiaji

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa litakutana baadaye mwaka huu kujadili suluhu ya wakimbizi na wahamiaji, lengo likiwa ni kuzileta pamoja nchi zote kuwa na mshikamano wa kibinadamu na mtazamo wa pamoja kuhusu suala hilo.

Hii ni mara ya kwanza baraza kuu la Umoja wa mataifa limeitisha mkutano huo wa ngazi ya wa wakuu wa nchi na serikali kujadili idadi kubwa ya wahamiaji na wakimbizi kuondoka sehemu moja kwenda nyingine na ni fursa ya kihistoria ya kuja na mtazamo wa pamoja na suluhu ya kimataifa ya kukabiliana na hali hiyo.

Mkutano huo wa siku nzima utafanyika Septemba 19 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York na umeandaliwa na Rais wa baraza kuu kwa niaba ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Filipo Grandi ni mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR

(SAUTI YA FILIPO GRANDI)

“Idadi ya watu ambao tunasema inatia wasiwasi, imeongezeka sana. Wanawake na wanaume, na hii ni idadi inayoshtua sana, na ni kubwa kuwahi kufikiwa tangu vita kuu ya pili ya dunia.”