Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya usalama yaimarika Burundi: UNHCR

Hali ya usalama yaimarika Burundi: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuimarika kwa usalama nchini Burundi kumeanza kutoa ahueni kwa wakimbizi ambao wengi wao wameanza kurejea nyumbani. Taarifa zaidi na Flora Nducha.

(TAARIFA YA FLORA)

Katika mahojiano na idhaa hii Mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini Burundi Abel Mbilinyi ameeleza kuwa juhudi za upatanishi za serikali na wadau wa ukanda zimeleta nuru kwani baadhi ya wakimbizi kutoka Tanzania wameanza kurejea nyumbani.

(SAUTI MBILINYI)

Mbilinyi amesema wakati kuna dalili njema za amani Burundi, UNHCR na wadau wanatoa hakikisho la misaada kwa wakimbizi wanorejea na wale walioko nchini humo.

(SAUTI MBILINYI)