Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito watolewa na viongozi kuziba pengo la kuhimili El Niño

Wito watolewa na viongozi kuziba pengo la kuhimili El Niño

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga UNISDR, Bwana Robert Glasser, leo amekaribisha wito kutoka kwa kundi la viongozi wa kimataifa wa kuziba pengo la dola bilioni 2.5 za ufadhili na kuinua uwezo wa kuhimi kmajanga, kwa nchi zinazohangaika na hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa, ukame na mmigogoro ya kibinadamu inayohusiana na El Niño.

Bwana Glasser amesema huu ni aina ya ujumbe ambao jumuiya ya kimataifa inapaswa kusikia. Hali mbaya ya hewa iliyosababishwa na El Niño kwa miongo sasa imeathiri takribani watu milioni 60, wakiwemo walio katika hali mbaya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Kusini Mashariki mwa Asia,Amerika ya Kati na Kusini na eneo la Pacific.

Ameongeza kuwa ni muhimu kuzisaidia nchi hizo sasa ili kujenga uwezo wa kukabili hatari ya majanga kwa ajili hatari zozote siku zijazo.

Kundi hilo la viongozi lilianzishwa na Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela mwaka 2007, na limetoa wito huo kabla ya mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika 19 Julai.

Kuna pengo la dola bilioni 2.5 za ufadhili baina ya fedha zinazohitajika iwa nchi zilizoathirika na El Niño