Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuelekea siku ya idadi ya watu duniani, vijana kuangaziwa

Kuelekea siku ya idadi ya watu duniani, vijana kuangaziwa

Kuelekea siku ya idadi ya watu duniani Julai 11, maudhui ya mwaka huu yakilenga uwekezaji kwa vijana, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA nchini Tanzania limeanza hamasa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kundi hilo ambalo ni zaidi ya nusu ya raia nchini humo.

Katika mahojiano na idhaa hii, Mwakilishi Msaidizi wa UNFPA nchini Tanzania Dokta Rutasha Dadi amesema shirika hilo linatarajia kutumia juma hili na siku ya kilele kujikita kwa vijana na changamoto na ustawi wao mathalani.

( SAUTI DK RUTASHA)

Kadhalika UNFPA ambayo inaratibu mikusanyiko ya vijana jijini Dar es salaam itaangazia mambo mengine.

( SAUTI DK RUTASHA)