Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mauaji ya wakili wa haki za binadamu Kenya

UM walaani mauaji ya wakili wa haki za binadamu Kenya

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani vikali mauaji ya wakili wa haki za binadamu nchini Kenya Bwana Willie Kimani, mteja wake Josphat Mwenda, na dereva wao wa taxi Joseph Muiruri, yaliyofanyika Juni 23, kwa tuhuma za kuendelea kwa mauaji yasiyo ya halali yanayofanywa na vikosi vya polisi. Grace Kaneiya na taarifa zaidi

(TAARIFA YA GRACE)

Watatu hao walitoweka baada ya Bwana Kimani na Bwana Mwenda kuhudhuria kesi mhakama ya Mavoko, kilometa 30 Mashariki mwa Nairobi, kesi inayomuhusisha afisa katika utawala wa polisi.

Mwenda alipigwa risasi na kuumizwa na polisi Aprili 2015 na kisha kufunguliwa mashtaka ya uongo ya uhalifu.

Willie Kimani, ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali la, International Justice Mission, alikuwa akimsaidia Mwenda katika kesi yake. Maiti zao zenye ishara ya kuteswa zimekutwa Juni 30 mtoni Kaskazini Mashariki mwa Nairobi. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu

(SAUTIO YA COLVILLE)

“Mwanasheria mkuu wa Kenya amesema kwamba hakuna jitihada zitakazoachwa ili kubaini wale waliohusika katika mauaji, na Inspekta Jenerali wa Polisi ametangaza kuwa uchunguzi wa kina utafanyika”