Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilimo kusalia tegemeo la ajira kwa vijana Afrika

Kilimo kusalia tegemeo la ajira kwa vijana Afrika

Ripoti mpya kuhusu mwelekeo wa kilimo duniani kwa mwaka 2016 hadi 2025 imetaja mambo yatakayobadili mwelekeo wa sekta ya kilimo katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara utaongezeka licha ya changamoto zinazokabili sekta hiyo.

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO na lile la Ulaya la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo (OECD katika ripoti yao wametaja mambo hayo kuwa ni kasi ya ongezeko la watu wa daraja la kati, kukua kwa miji na ongezeko la mvuto katika sekta ya kilimo.

Ripoti inasema sekta ya kilimo itakuwa chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana huku uagizaji chakula kutoka nje ukiongezeka sanjari na ongezeko la uzalishaji kwenye sekta ya kilimo.

Angel Gurría ni Katibu Mkuu wa OECD.

(Sauti ya Angel)

“Biashara ya bidhaa za kilimo itakuwa na dhima kubwa sana katika uhakika wa chakula katika ukanda huu. Kwa bahati mbaya ongezeko la utegemezi wa uagizaji chakula utaendelea barani Afrika. Kwa hiyo sera zote zinazosaidia kuimarisha biashara ya kikanda zinapaswa kuboreshwa Afrika iwapo tunataka kuwa na mazingira bora ya uhakika wa chakula.