Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa miaka mitano ya kukuza Kiswahili Afrika Mashariki waanzishwa

Mpango wa miaka mitano ya kukuza Kiswahili Afrika Mashariki waanzishwa

Wadau  mbalimbali wa lugha ya Kiswahili wamekutana hivi karibuni mjini Nairobi, Kenya na kupitisha  mpango mkakati wa lugha Kiswahili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mpango huo wa miaka mitano unanuwia kuimarisha matumizi  mapana ya lugha ya Kiswahili kwa kubuni  taasisi na asasi za Kiswahili katika nchi za Jumuiya ili kukuza na kueneza lugha hiyo ya kwanza ya  kiafrika inayozungumzwa na watu wengi .

Hata hivo  katika eneo hilo kumekuwa na changamoto ya viwango  vinavyotofautiana vya Kiswahili, Mkakati huo kati ya mambo mengi umechagiza kubadilishana kwa wataalamu na mitaala kama sehemu ya kusawazisha viwango hivyo. Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA alihudhuria kongamano hilona ametuandalia makala hii.