Ban alaani shambulizi la kigaidi Bangladesh

4 Julai 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani shambulizi la kigaidi lilifanyika jijini Dhaka, Bangladesh, mnamo Julai Mosi na Julai Pili.

Ban ametuma risala za rambi rambi kwa familia za wahanga, na kwa serikali na watu wa Bangladesh, huku akiwatakia uponaji wa haraka waliojeruhiwa.

Taarifa ya msemaji wake imesema kuwa Katibu Mkuu anatumai kuwa waliopanga na kutekeleza uhalifu huo watafikishwa mbele ya sheria.

Amesema anasimama imara katika mshikamano na Bangladesh, wakati inapokabiliana na tishio hilo la kigaidi, huku akisisitiza haja ya kuongeza juhudi za kikanda na kimataifa katika kuzuia na kupambana na ugaidi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud