Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji mkubwa wahitajika kupambana na kipindupindu Haiti

Uwekezaji mkubwa wahitajika kupambana na kipindupindu Haiti

Kuna haja ya kuwa na uwekezaji mkubwa katika mfumo wa afya nchini Haiti ili kushughulikia changamoto zinazowakabili wahudumu wa fya katika vita dhidi ya kipindupindu. Mwakilishi wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini humo Marc Vincent, ametoa kauli hiyo Ijumaa mjini Port-au-Prince.

Miezi 10 baada ya tetemeko kubwa la ardhi nchini humo la mwaka 2010 mlipuko wa kipindupindu ukazuka kwenye kisiwa hicho kwa mara ya kwanza bada ya karbu karne moja. Jopo la wataalamu huru likathibitisha kwamba mlipuko huo ulisababishwa na bakteria walioingizwa Haiti kutokana na shughuli za kibinadamu.

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa idadi ya visa vinavyokisiwa mwaka huu ni 13,000. Bwana Vincent anaelezea hali ya sasa na jinsi ugonjwa huo unavyoathiri watoto

(SAUTI YA MARC VICENT )

“Ndio, watoto bado wako hatarini na ugonjwa huu , nadhani haku kubwa zimepigwa katika kudhibiti ugonjwa na nadhani kazi zaidi inahitajika ili kuutokomeza ugonjwa huo na kuwalinda watoto. Na unajua kipindupindi ni ugonjwa unaosababishwa na maji, sio tuu kukabiliana na kipindupindi ni suala la kukabiliana na magonjwa yote yanayohusiana na maji ambayo ni chanzo cha pili kikubwa cha vifo vya watoto Haiti.”