Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajane, madhila na ustawi wao nchini Tanzania

Wajane, madhila na ustawi wao nchini Tanzania

Wajane!

Hili ni kundi ambalo linakumbwa na madhila kila uchao, halipewi umuhimu kwa utetezi wala uwakili. Hali hii imesababisha wajane wengi kudhalilishwa katika jamii zao, kupoteza samani zao na wengine pia kufanyiwa ukatili wa kimwili,kisaikolojia, kijinsia na kingono.

Kiuchumi wajane ambao wanatajwa kuwa takribani milioni 259 duniani kote wanaishi katika hali ya umasikini.

Ni takribani juma moja tangu dunia iadhimishe siku ya wajane Juni 23. Umoja wa Mataifa na wadau wa haki za binadamau wameitumia siku hii kuangazia mahitaji yaon a namna ya kuwakwamua.

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon amesema licha ya madhila wanayopitia mathalani ubaguzi kwa sababu ya umri na jinsia, wajane wazee wana rasilimali kidogo sana za kiuchumi baada ya maisha yao yote kufanya kazi ngumu ya bila malipo. Na hata katika nchi zilizoendelea Ban amesema thamani ya malipo ya uzeeni kwa wanawake inaweza kuwa asilimia 40 chini ya ile ya wanaume.

Licha ya hayo baadhi ya wajane wamechomoza kiuchumi hata baada ya kuwapoteza waume zao. Nchini Tanzania kwa mfano ambako kuna mpango maalum wa serikali kuwasaidia wajane kiuchumi, wako walioamua kutobweteka kwa kujitafutia kipato na kuwasomesha watoto wao.

Nicholas Ngaiza wa redio washirika  Kasibante Fm ya Kagera Tanzania amefunga safari kumtembelea mmoja wa wajane kielelezo. Ungana naye.